AfyaHabari

WAKAAZI LAMU WAHIMIZWA KUFUATA MASHARTI YA KUKABILI COVID 19

Wakaazi wa kaunti ya Lamu wamehimizwa kuendelea kuzingatia kanuni za kujikinga dhidi ya maambukizi ya virusi vya Corona.

Waziri wa afya katika kaunti ya Lamu Ann Gathoni amesema wimbi la tatau la maambukizi ya Corona linaonekana kuwa hatari zaidi hivyo na haifai kwa watu kulegeza kamba katika kupambana na ugonjwa huo.

Amesema kulingana na ripoti ya kitaifa ya hali ya maambukizi ya Corona wagonjwa wengi walioko katika vyumba vya watu mahututi ni wale wanaougua Corona.

Aidha amesema hadi kufikia sasa kaunti ya Lamu imefanyia vipimo vya corona watu zaidi ya 300 ambampo 10 kati yao wamepoteza maisha kutokana na maradhi hayo.

 

Guracho Salad