AfyaHabariKimataifa

RAIS WA TANZANI AFARIKI

Rais wa 5 wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli ameaga dunia.

Kifo cha Magufuli kimetangazwa rasmi Jumatano usiku na makamu wake Samia Hassan Suluhu ambaye amesema  rais Magufuli aliaga dunia katika hospitali ya Mzena iliyopo jijini Dar es Salam.

Suluhu amesema Magufuli amefariki mwendo wa saa kumi na mbili jioni saa za Afrika Mashariki kutokana na matatizo ya moyo.

Akithibitisha kifo hicho makamu wa rais Samia Suluhu amesema rais Magufuli alianza kuugua mnamo tarehe 14 mwezi Machi na kulazwa katika hospitali hiyo ambapo alifariki.

Magufuli ambaye ni rais wa tano wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania amefariki akiwa na umri wa miaka 61 na Kwa mda alijikuta katika macho ya ulimwengu baada ya Tanzania kuonekana kutofuata maagizo ya kudhibiti maambukizi ya virusi vya corona.

Kabla mara ya mwisho kuonekana hadharani na kuzua uvumi kwamba alikuwa akiugua virusi vya corona Magufuli alipinga kuwasilishwa chanjo ya Covid 19 nchini mwake.