HabariKimataifa

Samia Suluhu aapishwa rasmi kuwa rais wa Tanzania…

Samia Suluhu Hassan ameapishwa kuwa rais wa sita  wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania, na kuchukua kiti cha aliyekua rais Dkt Pombe Magufuli aliyeaga dunia jumatano machi 17 mwaka huu .

Samia  ameapishwa na jaji mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Hamis Juma, katika ikulu huko jijini Dar es Salaam.

Samia Suluhu  ameweka recodi mpya kuwa mwanamke  wa kwanza kuwa rais Afrika Mashariki.

Kadhalika mama SULUHU amechukua wadhfa  huo na atahudumu kwa kipindi kilichosalia cha muda wa urais hadi pale uchanguzi mwingine wa urais utakapofanyika.