HabariLifestyle

MAAFISA WA USALAMA KUPEWA BIMA YA AFYA.

Idara ya usalama nchini inasema inapania kuimarisha maisha ya maafisa wa usalama kwa kutoa bima ya afya itakayo wasimamia wanapogonjeka.

Kibito Wamuthuri afisa mkuu katika Ofisi ya Inspekta Jenerali wa polisi anasema serikali kwa sasa inajukumika kuhakikisha maafisa wote wanapata bima hiyo itakayo imarisha maisha yao.

Anasema bima hiyo inalenga kunufaisha maafisa wa magereza pamoja na maafisa wa polisi akisema tayari idara hiyo imetuma maafisa nyanjani kutoa hamasa kuhusu mpango huo.

Wakati huohuo afisa huyo amesema endapo afisa yeyote ataaga dunia akiwa kazini, bima hiyo itasimamia malipo ya fidia kwa familia ya afisa huyo.