AfyaHabari

KMPDU YASHINIZA SERIKALI KUKABILI AWAMU YA TATU YA CORONA.

Chama cha Madaktari nchini KMPDU sasa kinataka serikali kuweka mikakati mwafaka kukabili awamu ya tatu ya virusi vya corona.

Katibu mkuu wa KMPDUChibanzi Mwachoda amesema inasikirisha kuona hali ikizidi kuwa mbaya hata na zaidi katika hospitali za umma licha ya serikali za kitaifa na zile za kaunti kuahidi kuweka mikakati ya kukabili corona mwaka jana iwapo maambukizi yangeongezeka.

Haya yanajiri wakati waziri wa afya nchini Mtahi Kagwe akiagiza serikali zote nchini kuongeza  idadi ya vitanda vya wagonjwa na hata kuwarejesha madaktari ambao kandarasi zao zilikuwa zimeisha.

Hata Hivyo mwachonda ameshauri madaktari waliokuwa wameajiriwa kupitia mpango wa huduma ya afya kwa wote-Universal Health care kupuuza agizo hilo la serikali.

Mwachonda amesema madaktari hao walihangaika kutokana na ukosefu wa vifaa vya kujilinda dhidi ya maambukizi ya virusi vya corona katika kipindi cha miezi 6 walipoajiriwa.

Mwisho