Habari

Mtihani wa KCPE waanza kote nchini, huku usalama ukiimarishwa….

Takriban wanafunzi milioni 1.2 kote nchini wanafanya mtihani wa kitaifa wa darasa la nane KCPE leo.

Wanafunzi hao wameanza na somo la hisabati asubuhi kabla ya kufanya mtihani ya kiingereza lugha na baadae adhuhuri watafanya insha ya kiingereza.

Mwenyekiti wa baraza la kitaifa la mitihani KNEC Dkt John Onsati amewahakikishia watahiniwa wote wanaofanya mtihani wa KCPE kuanzia leo kwamba mitihani hiyo imelindwa, na karatasi za mitihani hiyo hazijaibiwa.

Akizungumza hapa Mombasa, Onsati amewashauri maafisa wa polisi kuwa wanaagalifu zaidi ili kuhakikisha hakuna udanganyifi wowote katika mitihani hiyo.

Ameongea haya katika eneo la uhuru na kazi baada ya kuongoza shughuli ya kufungua kontena ya mitihani.