AfyaHabariMombasa

Wakaazi 1400 Changamwe wanufaika na mpango wa kugharamia matibabu yao….

Jumla ya wakaazi elfu moja na mia nne kutoka eneo la changamwe wamenufaika na shilling million nane nukta nne kutoka kwa hazina ya maendeleo ya eneo bunge hilo ili kugharamia matibabu yao.

Akizungumza wakati wa kutoa hundi hiyo kwa walionufaika mbunge wa eneo hilo omar mwinyi amewahimiza wananchi ambao hawajajiandikisha katika bima ya afya kufanya hivyo na kuahidi kuwasajili wengine katika awamu nyengine mwaka ujao.

Wakati huo huo mwinyi amewahimiza wananchi kuendelea kuzingatia mashart ya kulinda dhidi ya maradhi ya corona wakati huu ambapo awamu ya tatu inaendelea kwa kasi kubwa.