HabariMichezo

UKOSEFU WA VIWANJA VYA MICHEZO WACHANGIA UTUMIZI WA MIHADARATI KAUNTI YA KILIFI …………….

Washika dau katika sekta ya Michezo kilifi kaunti wanataka uongozi wa kaunti hiyo kulizungumzia swala la ukosefu wa viwanja vya michezo.

Wakiongozwa na aliyekuwa mlinda lango wa kitaifa Mohamed Salim Magogo washika dau hao wanadai ukosefu wa viwanja hivyo umechangia ongezeko la utumizi wa dawa za kulevya.

Wakati huo huo aliyekuwa mwenyekiti wa KFF tawi la Kilifi  Jamal Rais kwa jina la kiutani Bachelor Boy ameomba uongozi wa kaunti hiyo kuelezea hadharani mmiliki wa uwanja wa Bukungu al-maarufu Karisa Maitha.

Haya yanajiri wakati ambapo kumekuwa na taarifa za kuboreshwa kwa uwanja wa Water Bila mafanikio.