AfyaHabari

Mbunge wa Kiambaa Paul Koinange amefariki dunia mapema leo alipokuwa akitibiwa ugonjwa wa Covid-19.

Familia ya marehemu imesema Mbunge huyo amefariki katika Hospitali ya Nairobi.

Koinange alikuwa mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Utawala na Usalama wa Kitaifa na alichaguliwa kwa tiketi ya chama cha Jubilee.

Rais Kenyatta ametuma rambi rambi zake kwa familia ya Koinange akimtaja kama kiongozi aliekuwa na mchango mkubwa katika agenda ya amani ya serikali.