Habari

Mwanahabari wa shirika la KBC auawa kwa kupigwa risasi……..

Imebainika kwamba  mshukiwa aliyemuua mwanahabari wa shirika la KBC alipiga simu punde tuu baada ya kutekeleza mauaji hayo nyumbani kwake huko Ololua Kajiado.

Polisi wanasema kabla ya kumuua Betty Barasa, mshukiwa aidha alikuwa anapiga simu ikionekana kuwa alikuwa anapokea maagizo kutoka kwa mtu Fulani.

Polisi wanasema Barasa alipigwa risasi kichwani mara mbili jana jioni alipokuwa anatoka kazini.

Inaarifiwa marehemu ambaye pia ni mhadhiri katika chuo kikuu kimoja, aliondoka kazini saa moja na nusu jioni na kufika nyumbani kwake saa mbili na nusu, alifumaniwa na washukiwa watatu wa ujambazi alipokuwa akiregea nyumbani na kuingia nae ndania ambapo kisha waliwaamuru wanawe kulala chini .

Inaarifiwa kwamba washukiwa hao wa ujambazi walimuamuru Betty kuwapa fedha kisha kumuelekeza katika chumba kingine kwenye nyumba hiyo alimokuwa mumewe na kuwapokonya simu za rununu na vipatakalishi baada ya hapo walimpiga risasi katika chumba tofauti na kutoweka.

Mwili wake unahifadhiwa katika hifadhi ya maiti ya Montezuma huku uchunguzi ukiendelea.