AfyaHabari

Usalama wa chanjo ya Astrazeneca wazidi kutiliwa shaka……….

Usalama wa chanjo dhidi ya virusi vya Corona ya Astrazeneca unazidi kutiliwa shaka, baada ya utafiti uliofanywa barani Uropa kubainisha kwamba inahusika pakubwa na mgando wa damu miongoni mwa waliochanjwa.

mamlaka ya udhibiti utumizi wa dawa barani humo EMA imesema iliwafanyia utafiti watu waliokuwa na mgando wa damu kwenye ubongo na ambao tayari walikuwa wamepewa chanjo ya Astrazeneca.

Kufikia sasa kuna watu 169 walioripotiwa kuwa na mgando wa damu barani Uropa baada ya kuchanjwa watu milioni 34.

mamlaka hiyo sasa imewashauri maafisa wa afya na wale wanaochanjwa kuwa makini kufuatia athari hiyo ya mgando wa damu ambayo huripotiwa baada ya wiki mbili mtu anapopewa chanjo.

baadhi ya mataifa kama vile Uholanzi yamesitisha kutoa chanjo hiyo kwa raia wake haswa wenye umri wa chini ya miaka 60 kwani ndio wanaoathirika zaidi.