AfyaHabariMombasa

Huduma za maji zatatizika hapa Mombasa baada ya bomba kupasuka….

Huduma za usambazaji maji katika maeneo ya Kisauni na kisiwani hapa Mombasa zimetatizika baada ya bomba la kusambaza maji kupasuka katika eneo la Baricho katika kaunti ya Kilifi.

Kulingana na taarifa ya kampuni ya usambazaji maji ya Mombasa MOWASCO, shughuli hizo zitatatizika kwa muda huku ikibaini kwamba tayari bomba hilo limeanza kukarabatiwa.

Haya yanajiri huku wakaazi wa kaunti ya Mombasa wakilalamikia uhaba wa maji wa mara kwa mara  huku wakitaka kampuni husika kuingilia kati kutatua ukosefu wa bidhaa hio muhimu.