BurudaniEntertainment

MSANII HARUN DEE AINGIA STUDIO NA WALINZI/MABOUNCER

Harun Dee Msanii aliye chini ya Uongozi wa Akothee Empire, siku ya Ijumaa alishangaza Wengi baada ya kuingia Studio aliyokuwa ameitwa kufanyiwa mahojiano akiambatana na Walinzi/Mabouncers.

Akielezea kuhusu walinzi hao Harun alisema kuwa na Walinzi kwa msanii kama mimi si kitu kigeni na kuwa ni moja wapo ya mahitaji ya msanii yeyote yule. Ikumbukwe kuwa Harun Dee Aliingia Akothee Empire baada ya Msanii Ziki Mtana kutemwa kutoka lebel hiyo. Kwa sasa Harun anatamba na wimbo Nikomeshe

By: Yussuf Tsuma