HabariMazingira

Halmashauri ya bahari KMA kuanzisha kampeni ya kusafisha bahari

Halmashauri ya masuala ya bahari KMA inalenga  kuanzisha kampeni ya kusafisha bahari  ili kukabiliana na uchafuzi wa mazingira.

Akizungumza na wandishi wa habari mkurugenzi wa halmashauri hiyo Robert Njue amesema halmashauri hiyo ina jukumu kubwa la kuhakikisha kwamba hakuna uchafuzi wa bahari hindi,hatua ambayo imewapelekea kuleta mashirika mbali mbali pamoja ili kufanikisha zoezi hilo.

Mkurugenzi huyo aidha anadai kwamba iwapo hatua ya mapema haitochukuliwa basi hali ya bahari hiyo itasalia kuwa mbaya jambo ambalo huenda likasababishia wavuvi kukosa kazi kwani idadi ya plastiki zilizoko ndani ya bahari hindi inazidi kuongezeka.

Kampeni hiyo inanuia  kuhusisha kaunti sita za Pwani  huku magavana wa kaunti hizo wakitarajiwa kuhudhuria mkutano wa siku ili kujadili swala hilo.

Gavana wa Mombasa, Kwale,  lamu na Kilifi ni miongoni mwa viongozi watakaoongoza zoezi hilo.

 

By Reporter David Otieno