AfyaHabari

Mshukiwa wa ulanguzi wa dawa za Kulevya Voi aendelea kutibiwa…………

Mshukiwa wa ulanguzi wa dawa za kulevya anaendelea kutibiwa katika hospitali ya rufaa ya Voi katika kaunti ya Taita Taveta baada ya kumeza dawa aina ya Heroin.

Polisi wamesema mshukiwa huyo kwa jina  Pualine Mogore  mwenye umri wa miaka 48 alimeza dawa hizo kwa haraka alipowaona maafisa wa polisi ili kukwepa kukamatwa huko Voi.

Aidha polisi wamesema wamefanikiwa kupata dawa nyingine zaidi za kulevya baada ya kufanya msako nyumbani kwake.

Na tukisalia kwenye kaunti hiyo ni kwamba maafisa wa kulinda na kuhifadhi wanyamapori nchini KWS kaunti ya Taita Taveta wanamzuilia mwanaume mmoja baada ya kupatikana na pembe ya ndovu katika eneo  la Elerai mbuga  ya Tsavo Mashariki.

Mwanaume huyo kwa jina Papayo Olekisoi alikamatwa na maafisa hao baada ya ndovu mmoja kuuwawa mwezi moja uliopita katika eneo la Losito kabla mshukiwa kuenda mafichoni.

Aidha maafisa hao wamesema mshukiwa alikamatwa baada ya ushirikiano na maafisa wa nchi jirani ya Tanzania ambako inaaminiwa pembe moja ilivukishwa nchini humo.

By Reporter Aisha Juma