AfyaHabari

Serikali yahimizwa kutilia mkazo masharti ya corona huko Malindi………….

Viongozi wa kidini mjini Malindi kaunti ya Kilifi sasa wanaitaka serikali kuweka mkazo zaidi katika masharti yaliyowekwa kudhibiti maambukizi ya virusi vya Corona eneo hilo.

Wakiongozwa na mwenyekiti wa SUPKEM eneo hilo Ustadh Aboud Salim viongozi hao wanadai kuwa maafisa husika wamelegeza kamba katika kuhakikisha kuwa masharti ya wizara ya afya yanafuatiliwa ipasavyo.

Kulingana na Salim wakaazi wengi mjini Malindi kwa sasa hawafuati sheria za vitengo husika akisisitiza haja ya hatua mwafaka kuchukuliwa ili kuzuia maambukizi zaidi.

Ni kauli ambayo imeungwa mkono na kasisi Wilbert Lago wa jimbo katoliki eneo la Malindi.

Lago amesema kuwa ni jukumu la kila mmoja kujikinga dhidi ya ugonjwa wa Corona na kutopuuza athari zinazoletwa na ugonjwa huo.

Viongozi hao waliyasema hayo baada ya kushiriki dhifa ya iftar iliyoandaliwa na Kasisi Wilbert Lago iliyoandaliwa katika makao makuu ya kanisa katoliki mjini malindi.

By Correspondent Joseph Yeri