AfyaHabari

Rais Uhuru Kenyatta asitisha marufuku ya kuingia na kutotoka nje katika kaunti tano zilizopigwa marufuku ya usafiri kama njia mojawapo ya kudhibiti msambao wa virusi vya korona.

Akihutubia wananchi masaa machache katika ukumbi wa rais  jijini Nairobi kwenye hafla ya siku ya wafanyikazi yaani Leba Day , Rais Uhuru kenyatta amesema  kwamba kutokana na ushauri kwa wadadisi katika masala ya usalama , afya na uchumi, agizo hilo limedhibiti kiwango cha kusambaa kwa virusi hivyo kwa asilimia 74.

Wakati huo huo rais kenyatta amepunguza masaa ya kutotoka nje nyakati za usiku maarufu kafyu kuanzia saa nne usiku hadi 10 alfajiri katika kaunti tano zilizofungwa , huku sehemu za ibada zikipata nafuu za kuendelea maombi japo chini ya masharti ya kudhibiti korona.

Aidha katibu mkuu wa wafanyikazi nchini Francis Atwoli amewasihi wamailiki wa maduka makuu kuwapa wafanyikazi wao lisali moja ya kuweza kupunguza wakiwa katika jukumu la kuhudumia wakenya kwenya maduka hayo.

By News Desk