Habari

Wakaazi wa kijiji cha Kanyangwa Kaunti Ya Kilifi Waachwa Bila Makao

Mamia ya wakaazi katika kijiji cha Kanyangwa huko Furunzi eneo bunge la Malindi kaunti ya Kilifi wameachwa bila makao baada ya makaazi yao kuvunjwa usiku wa kuamkia leo.

Kulingana na baadhi ya waathirika  ni kwamba ubomozi huo umetekelezwa mwendo wa saa kumi na moja asubuhi chini ya ulinzi mkali wa magari ya polisi.

Baadhi ya viongozi waliofika eneo la mkasa wamelaani vikali ubomozi huo wakidai haukuzingatia sheria.

Wakiongozwa na Mbunge wa Malindi Aisha Jumwa na Mwakilishi wa Wadi ya Malindi mjini Kadenge Dadu,viongozi hao wamevitaka vyombo vya dola kukoma kutumiwa na mabwenyenye kuhangaisha wakaazi eneo hilo.

Hata hivyo naibu kamishena kaunti ndogo ya Malindi Thuo Ngugi amesema japo kamati yake ya usalama inafahamu kuhusu ubomozi huo agizo la mahakama limepitia kwa kamanda wa polisi kaunti hiyo

By News Desk