HabariSiasa

Tume ya huduma za mahakama JSC kuaaanza  mahojiano ya kumtafuta jaji wa mahakama ya upeo tarehe tatu mwezi wa tano mwaka huu……………

Tume ya huduma za mahakama JSC itaanza  mahojiano ya kumtafuta jaji wa mahakama ya upeo hapo kesho, hii ni baada ya mahakama ya rufaa kutupilia mbali uamuzi wa awali wa mahakama kuu kusitisha mahojiano hayo

Kwa mujibu wa ratba hiyo Jaji Said Chitembwe na Jaji Marete Njagi watahojiwa siku ya kesho kuanzia saa tatu, jumanne itakuwa zamu ya Jaji Nduma Nderi na dkt Nyaberi Patrick Lumumba

Siku ya jumatano makamishna wa JSC watawahoji  majaji William Ouko, Joseph Kiplagat Sergon na Alice Yano.

Watu tisa walikuwa wametuma maombi ya kutakaa kuteuliwa kuwa jaji wa mahakama ya juu, lakini ni saba tu watakaohojiwa kwani Jaji Martha koome ameteuliwa kuwa jaji mkuu naye Minoti Kathurima alijiondoa.

Na Meza  Ya Habari