HabariMombasaSiasa

Wakenya wahimizwa kutochagua viongozi kwa misingi ya vyama…….

Mwaniajai wa kiti cha eneo bunge la  jomvu karisa Nzai amewasihi wakenya kuchagua viongozi kwa kutoaangazia misingi ya vyama venye umaarufu bali kuangazia maono yao.

Akizungumza katika kipindi sauti asubuhi Nzai amesema kuwa taifa limekuwa na chanagamoto si haba kutokana na uongozi duni unayosabibishwa na wanasiasa ambao wanachaguliwa kwa misingi ya vyama bali sio kwa rekodi zao za utendakazi.

Ameongeza kuwa iwapo wakenya watabadili fikra hiyo basi taifa litaanza kuendelea kimaendeleo kwani kuna viongozi wanao na uwezo bali wamefungiwa nje kwa sababu ya kutoshabikia vyama maarufu.

Wakati huo huo kiongozi huyo amewahakikishia wanati wa jomvu ajira kwa vijana iwapo atapewa nafasi ya kuwawakilisha katika bunge la kitaifa katika uchaguzi mkuu ujao.

By Reporter David Otieno.