HabariLifestyle

Serikali yatakiwa kuwekeza zaidi katika elimu ya watu wazima…..

Serikali kupitia wizara ya elimu imetakiwa kuwekeza zaidi katika elimu ya watu wazima baada ya sekta hiyo kuonekana kukumbwa na changamoto si haba na ambayo inaendelea kuvutia watu wengi waliokosa nafasi ya masomo wakiwa  na umri mdogo

Kulingana na Leonard Kevin Mwende mmoja wa walimu ni kuwa uhaba wa walimu na maeneo ya kuwapa mafunzo wanafunzi wao ni baadhi tu ya changamoto wanazokumbana nazo.

Hata hivyo idara hiyo inategemea wafadhili mbalimbali ili kuwapa mafunzo wanafunzi hata baada ya kuanzishwa na serikali 1979.

Aidha kulingana na afisa mkuu wa elimu ya watu wazima eneo la Changamwe na Jomvu Grace Wambete, ni kwamba matarajio yao ni kuwa na wanafunzi zzaidi ya 1,500 na amewtaka viongozi kuwahimiza wakaazi kujitokeza na kupata mafunzo hayo.