HabariMazingiraMombasa

Makundi ya uhalifu yaanza kusakwa kaunti ya Kwale…..

Idara ya usalama kaunti ya Kwale imeanzisha oparesheni ya kuyasaka makundi ya vijana ya kihalifu yanayowahangaisha wakaazi wa kaunti hiyo.

Kamishna wa kaunti hii Joseph Kanyiri amesema kuwa oparesheni hiyo inalenga kuyakabili kisheria makundi hayo yanayoonekana kuchipuka tena.

Kanyiri amesema kuwa oparesheni hiyo inatekelezwa na maafisa wa polisi katika maeneo mbali mbali yaliyokithiri visa vya uhalifu.

Wakati uo huo  amewataka wazazi kuwalinda wanao dhidi ya kujiingiza katika makundi  hayo haramu.

Kanyiri ameonya kuwa vijana watakaopatikana wakijihusisha na makundi hayo watachukuliwa hatua kali za kisheria.