HabariLifestyleMombasa

Wakaazi wa Jomvu hapa Mombasa walilia haki zao za ardhi……..

Wakazi wa Jomvu kuu eneo bunge la Jomvu kaunti ya Mombasa wanalilia haki kutokana na dhulma za historia ya ardhi yao ya zaidi ya hekari 105 ambayo wanadai  kuwa wanapokonywa na kanisa moja eneo hilo.

Akizungumza na meza yetu ya habari msemaji wa jamii hiyo Kombo Ahmed Kombo anasema wanazidi kunyanyaswa kiasi cha kuwa wengine wao wanatishiwa maisha  huku  wengine wakikamatwa bila makosa yoyote.

Kulingana na joyce Sabiki mmoja wa wenyeji eneo hilo,kukamatwa kwa Axuel Lameck kumewatia uoga kwani hakuna anaejuwa zamu yake ya kukamatwa, huku akisema licha ya wao kuzidi kutafuta haki zao viongozi wa kanisa hilo wanaendelea kuwanyanyasa hata baada ya kushinda kesi mahakamani.

Kwa sasa wakazi hao wanatoa wito kwa wadau husika kuingilia na kuwanusuru mikononi mwa kanisa hilo huku wakimyeshea kidole cha lawama mbunge wa eneo hilo Badi Twalib .