HabariSiasa

Shughuli ya kumsaka jaji atakayejaza nafasi ya Jaji Jackton Ojwang yaingia siku ya pili…

Shughuli ya kumsaka jaji atakayejaza nafasi ya Jaji Jackton Ojwang aliyestaafu katika mahakama ya juu inaendelea kwa sasa ambapo jaji Nduma Ndeari ameendelea kutetea utendakazi wake katika idara ya mahakama hasa katika kushughulikia   kesi za ufisadi vile vile maswala ya jinsia.

Jaji Nderi amesema kwamba amefanya maamuzi katika kaunti ambapo amezingatia sheria, haki na maadili katika jamii na kutaja uzoefu huo kuwa muhimu anapolenga kuwa jaji wa mahakama ya juu .

Nderi aidha ametakiwa kufafanua uelewa wake kuhusu majukumu yanayostahili kutekelezwa na mahakama ya juu ambapo amesema miongoni mwa majukumu hayo nikuhakikisha kwamba kesi mbali mbali za uchaguzi zinashughulikiwa kwa wakati.

Baadae itakuwa zamu ya jaji Patrick Lumumba kuhojiwa na makamishna wa JSC.