HabariSiasa

Afueni kwa spika wa bunge la kaunti ya tanariver baada ya mahakama kusitisha mchakato wa kumtimua malakani…….

Spika wa bunge la kaunti ya Tanariver Justin Kaduda amepata afueni ya muda baada ya mahakama inayoshughulikia mizozo ya wafanyakazi katika kaunti ya mombasa kusitisha mchakato wa kumtimua mamlakani.

Jaji Brian Ongaya amewaagiza mawakili wa kaduda kuwasilisha nakala maalum kutoka kwa mahakama hiyo katika bunge ya  Tanariver kabla tarehe 14 mwezi huu.

Jaji Ongaya pia amewaagiza mawakili wa bunge hilo kuwasilisha majibu yao mbele ya mahakama hiyo kufikia tarehe 25 ya mwezi uu huu kabla ya kesi hiyo kuanza kuskilizwa tarehe mbili mwezi ujao.