HabariMazingira

Wakaazi kutoka eneo la Hewani kaunti ya Tana River wamenufaika kwa kupata maji safi…

Wakaazi kutoka eneo la Hewani kaunti ya Tana River wamenufaika kwa kupata maji safi kupitia mradi wa maji   kutoka kwa shirika lisilo la kiserali.

Hii ni baada ya  wakaazi  hao takriban 6,000  kulalamikia uhaba huo wa maji kwa miaka mingi sasa vilevile kusema kuwa limekuwa tatizo kubwa kuteka maji kutoka mto Tana kwani ni mbali sana na makao yao.

Aidha wamesema kuwa wengi wao wamepoteza maisha na wengine kujeruhiwa vibaya wanapoenda kuteka maji na kushambuliwa na mamba na viboko.

By Aisha Juma