Habari

Familia moja imewapoteza watu watano kufwatia ajali ya barabarani ……..

Hii ni baada ya gari hilo kugongana na trela katika eneo la Taru barabara kuu ya Nairobi Mombasa mapema hii leo .

Kwa mujibu wa afisaa mkuu wa polisi wa Trafiki Mombasa Peter Maina ajali hiyo ya saa kumi na moja leo asubuhi ilitokea baada ya trela hilo lililo kuwa likijaribu kuyapita magari mengine kugongana ana kwa ana na gari hilo la Vokx lililokuwa likitoka upande wa pili na kusababisha vifo vya watu watano papo hapo.

Aidha abiria wengine wanne wanaendelea kupokea matibabu katika hospitali ya Kinango.