AfyaHabariNews

Kilifi yaorodheshwa nambari tatu kwa maambukizi ya malaria nchini…..

Kaunti ya Kilifi inaorodheshwa nambari ya tatu kati ya kaunti zenye idadi kubwa ya maambukizi ya ugonjwa wa malaria nchini.

Kulingana na waziri Charles Dadu, wadi ya Kambe Ribe eneo bunge la Rabai imeorodheshwa ya tatu kitaifa kuwa na maambukizi ya juu ya ugonjwa wa Malaria nchini.

Dadu amesema wameweka mikakati ya kupambana na ugonjwa huo ili kupunguza ongezeko la idadi kubwa ya visa hivyo vinavyoripotiwa kaunti ya Kilifi.

Hata hivyo Dadu amesema shughuli ya ugavi wa vyandarua vya kujikinga mbu litaongezwa muda kufuatia kaunti ya Kilifi kupokea vyandauwa hivyo kwa awamu.

Aidha amesema kuwa kila mkaazi aliyeandikishwa atapata vyandaruwa hivyo na idadi kamili ya vyandarua ili waweze kujikinga na maambukiza ya ugonjwa wa malaria.

By Ericson Kadzeha