HabariNews

Waendeshaji bodaboda Kilifi wako kwenye hatari ya kukabiliwa kisheria…..

Mwenyekiti wa bodaboda hapa kaunti ya Kilifi Joseph Mwango ameweka wazi kuwa wanaoendesha pikipiki hizo, wapo katika hatari ya kukabiliwa na sheria katika kazi yao, kutokana na baadhi ya mizigo wanayo tumiwa ili kusafirisha kutoka sehemu moja kuelekea nyingine.

Akizungumza na wanahabari amesema kuwa wakati mwingi madereva hupewa kazi ya kusafirisha bahasha kutoka sehemu tofauti, na kuzifikisha katika maeneo  wanayoagizwa pasi na kujua kilicho ndani, swala ambalo amelitaja kuwa hatari kwani hatimaye wengi hujipata na bidhaa haramu ambazo hufichwa ndani ya bahasha hizo..

Kauli hio imeungwa mkono na Famau Muhammed Famau, mwanaharakati wa kukabiliana na dawa za kulevya kaunti ya Kilifi, ambaye amehoji kuwa madereva hao hupewa kiasi kikubwa cha fedha, katika kutekeleza kazi hio pasi na kujua malengo ya wale wanao waagiza, na kuwapelekea baadhi yao kutiwa mbaroni na maafisa wa polisi, baada ya kupatikana na bidhaa haramu.

By Joseph Yeri