HabariSiasa

Charles Owino ahamishwa kutoka wadhfa wa msemaji wa polisi….

Msemaji wa tume ya huduma kwa polisi Charles OWINO amehamishwa kutoka kwa wadhfa huo katika mageuzi ya hivi punde yaliyotangazwa na inspekta generali wa polisi.

Tume hiyo sasa inatafuta msemaji mpya wa polisi baada ya Owino kuhamishwa hadi kitengo cha kitaifa cha kusimamia silaha ndogo ndago cha Nationa Focal Point on small arms and light weapons ambapo amepewa wadhfa wa naibu mkurugenzi wa kitengo hicho cha kitaifa.

Miongoni mwa wale ambao wanatazamiwa kuchukua wadhfa wa Owino, ni naibu msemaji wa tume hiyo Charles Kosgey, na kamanda wa kaunti ya Transnzoia Fredrick Ochieng.

By News Desk