HabariTravel

Mamlaka ya viwanja vya ndege yasitisha safari za ndege kati ya Kenya na Somalia……….

Mamlaka ya kusimamia viwanja vya ndege nchini KCAA imesitisha safari zote za ndege kati ya taifa la Kenya na taifa jirani la Somalia

Mamlaka hiyo aidha inasema hatua hii imechukuliwa kutokana na habari muhimu na zinazohitaji uzito unaofaa.

Marufuku hii  inajiri siku chache baada wizara ya mawasiliano nchini Somalia kusema kuwa mataifa hayo mawili yamekubali kufanya kazi kwa pamoja na kuweka uhusiano wa kirafiki kwa misingi ya kanuni za kuheshimiana na uadilifu, kutokuingiliana katika maswala ya kindani, usawa, kunufaishana na kuishi kwa Amani.

Hii ni baada ya taifa la Qatar kuingilia kati kuona kuwa mahusiano baina ya mataifa hayo mawili yanarudi sawa.

By News Desk