AfyaHabari

Idara ya afya Kilifi yaweka mikakati ya kuzuia maambukizi ya Corona magerezani…….

Waziri wa afya Kaunti ya kilifi Charles Dadu amesema Idara ya afya Kaunti hiyo imeweka mikakati kabambe ili kudhibiti maambukizi ya virusi vya Covid-19 hususan Katika magereza.

Kulingana na Dadu hali hii imejiri baada ya idadi kubwa ya maambukizi kuonekana kutoka katika magereza Katika Kaunti hiyo.

Dadu amesema gereza la Malindi limeonekana kuongoza pakubwa Katika maambukizi hayo ikizingatiwa kuwa linahudumia eneo kubwa la mkoa wa pwani.

Dadu ameeleza kuwa wameshirikiana na usimamizi wa magereza Katika kuweka miundo msingi ambayo itasaidia Katika kupambana na maambukizi ya virusi hivyo.
Dadu amesema ujenzi wa zahanati Katika gereza hilo ni miongoni mwa mikakati iliyowekwa.

By Kilifi Correspondent Erickson Kadzeha.