AfyaHabari

Waathiriwa wa HIV Taita wahimizwa kutembelea kliniki zao……..

Serikali ya kaunti ya Taita Taveta imewahimiza waathiriwa wa virusi vya HIV na ukimwi kutembelea kliniki zao ili kuendelea kupokea huduma za afya zikiwemo  dawa na ushauri kupitia mafunzo ya kliniki

Mshirikishi wa maswala ya HIV kaunt hiyo Charity Mwabili anasema huduma zinazotolewa kwa waathiriwa hao zinaendelea katika hospitali zote za umma ilicha ya kuwepo kwa janga la Corona

Mwabili aidha ameongeza kuwa wamezingatia masharti yote ya wizara ya afya ya kuzuia msambao wa virusi vya Corona wakati wa kliniki za waathiriwa wa virusi vya Ukimwi.

By Reporter Joyce Mwendwa