HabariSiasa

Hatma ya mchakato wa BBI kujulikana Ahamisi, mahakama kutoa uamuzi………

Bunge la seneti hii leo linatarajiwa kupigia kura mswaada wa marekebisho ya Katiba,

Siku ya ijumaa bunge la kitaifa lilipitisha mswaada huo kwa kukubali marekebisho kufanywa.

Haya yanajiri huku majaji 5 wakitarajiwa kutoa uamuzi wao siku ya Alhamisi iwapo  kura ya maamuzi itaandaliwa, hii ni baada ya kesi 7 kuwasilishwa mahakamani kupinga mchakato wa BBI.

Kesi hizo ziliwailishwa na mwanauchumi David Ndii, Muungano wa wauguzi, chama cha Third Alliance, 254 Hope, Justus Juma, Moraa Omoke, Isaac Aluochier na shirika la kuetea haki za kibinadamu la MUHURI.

Majaji hao ambao watatoa uamuzi wao ni pamoja na Jaji Joel Ngugi, George Odunga, Jarius Ngaah, Janet Mulwa na Chacha Mwita.

By Reporter Joyce Mwendwa…