HabariNews

Washukiwa wawili wa kundi la Alshabaab wauawa huko Wajir……….

Washukiwa wawili wa kundi la kigaidi la Al-Shabaab wameuawa katika eneo la Tarbaj kaunti ya Wajir.

Maafisa kadhaa wa polisi wanaripotiwa kujeruhiwa kwenye shambulizi hilo. Kulingana na polisi eneo hilo wanamgambo hao walikuwa wanajaribu kuharibu mlingoti wa mawasiliano ya simu wa Telkom.

Kamanda wa polisi kaunti ya Wajir Hillary Rotich anasema makabiliano yalizuka kati ya wanamgambo hao na maafisa wa polisi kabla ya washukiwa haokupigwa risasi.

Hata hivyo Rotich amesema oparesheni imeanzishwa ya kuwasaka wanamgambo zaidi huku akitoa wito kwa wananchi kuwa waangalifu haswa wakati huu wanapojiadaa kusherekea siku kuu ya EID.

BY Joyce Mwendwa…