HabariNewsSiasa

EACC yatakiwa kuchunguza wizara ya maji Kilifi………

Mwakilishi wa Wadi ya Ganze kaunti ya Kilifi Benson Chengo sasa anaitaka tume ya kupambana na ufisadi Nchini EACC kuchunguza wizara ya maji kwa madai ya utepetevu unaochangia kudorora kwa huduma za usambazaji maji eneo hilo.

Chengo amedai kuwa baadhi ya wafanyikazi wa kampuni ya maji eneo hilo KIWASCO hawajalipwa mishahara yao kwa miezi minne sasa, kutokana na mipangilio duni ya uongozi.

Chengo amesisitiza kuna haja ya uchunguzi kufanywa haraka iwezekenavyo ili kubaini kiini cha shida hiyo huku akiongeza kuwa jambo hilo limesambaratisha huduma za maji eneo hilo.

Vile vile Chengo anadai kuwa wizara hiyo iliajiri maafisa zaidi katika sekta hiyo na kufinyilia bajeti ya mishahara ya wafanyikazi hao.

Chengo aidha ameongeza kuwa shughuli ya kuajiri wafanyikazi haikuhusisha bodi ya uajiri ya kaunti ya Kilifi.

Akizungumza kwa njia ya simu katibu katika wizara hiyo Kennedy Kazungu amepuzilia mbali madai hayo na kusisitiza kuwa wafanyikazi wa sekta hiyo wamekuwa wakilipwa mishahara yao na kuwa hana taarifa yoyote kuhusu madai hayo.

By Correspondent Joseph Yeri.