AfyaHabariMombasa

Serikali ya Mombasa yahimizwa kuweka kliniki tamba eneo la Mwakirunge…

Familia zinazoishi kwenye jaa la taka kule Mwakirunge  zinatoa wito kwa uongozi wa kaunti ya Mombasa kupitia idara ya afya kubuni  zahanati tamba ama( mobile clinic) zitakazowapa huduma za matibabu kila wanapougua.

Hii ni baada ya familia hizo kulalamika kwamba mara nyingi hukosa matibabu wakati wanapougua  kutokana na magonjwa yanayosababishwa na mazingira machafu wanayoishi.

Wakaazi hao wameongeza kuwa hospitali zipo mbali hivyo basi wameitaka serikali kuingilia kati na kuwasaidia.

By Reporter Gladys Marura