HabariNewsSiasa

Sammy Lishore ateuliwa kuwa seneta mteule…..

Aliyekuwa seneta wa Samburu Sammy Leshore ameteuliwa na chama tawala Jubilee kuwa seneta mteule kuchukua nafasi ya Issack Mwaura.

Hii ni baada ya spika wa seneti  Ken Lusaka kutangaza hapo jana kuwa nafasi ya Mwaura ya seneta mteule imewekwa wazi,pia hii ni licha ya mahakama kuagiza seneti kutomwondoa Mwaura kutoka wadhfa wake hadi rufaa aliyowasilisha itakapo sikilizwa na kuamuliwa.

Tayari IEBC imeorodhesha jina la Sammy Leshore kwenye gazeti rasmi la serikali kama seneta mteule kutoka chama cha jubilee ambae anawakilisha watu wanaoishi na ulemavu kufuatia kutimuliwa kwa seneta Issac Mwaura.

By Reporter Gladys Marura