HabariMombasa

Wakaazi Mombasa watakiwa kutochukua sheria mikononi mwao…

Kamishna wa kaunti ya Mombasa Gilbert Kitiyo ametoa wito kwa wakaazi wa Mombasa kutochukua sheria mikononi mwao kwa kuchoma wahalifu wanapowakamata huku akiwashauri kuwapeleka  katika kituo cha polisi ili haki itendeke.

Akizungumza katika kipindi cha sauti asubuhi hii leo kupitia njia ya simu baada ya video  kusambaa mitandaoni inayoonesha vijana  wanaoaminika kuwa ni wahalifu kutoka kikundi cha wakali kwanza kuchomwa na kupigwa vibaya eneo la bamburi .

Aidha ameongeza kwanza kamati ya usalama kaunti hiyo imeweka mikakati thabiti kuwahakikishia wananchi usalama kwani hata maafisa wa usalama pamoja na machifu na manaibu tayari wamehamashishwa kuhusiana na swala hilo.

By David Otieno