HabariMombasa

Maandamano ya kupinga hujuma dhidi ya Palestine yaendelea hapa Mombasa……..

Maandamano ya kupinga hujuma wanazofanyiwa raia wa Palestine na utawala wa kizayuni wa Israel yameendelea hapa Mombasa kwa siku ya tatu mfululizo kupinga hujuma hizo.

Hii leo kikundi cha vijana kimekusanyika katika eneo la treasury square hapa Mombasa wakipinga hujuma hizo zinazofanyiwa wapalestina na waisraeli kwenye ukanda wa gaza.

Wakiwa wamekaa chini huku wakiwa wameinua mabango na kushikililia maua, vijana hao wamesema kwamba nia yao sio kuzua rabsha bali bali kuhubiri Amani ili kumalizika kwa hujuma hizo.

Aidha vijana hao wametumia fursa hio kukumbushana maandiko matakatifu kwenye vitabu vya dini ya kiislamu.

By reporter Nick Waita