HabariMichezoMombasa

 Awamu ya pili ya kuurekebisha uwanja wa Michezo wa freeretown eneo bunge la Nyali yaanza rasmi………..

Awamu ya pili ya kuurekebisha uwanja wa Michezo wa freeretown ulioko eneo bunge la Nyali imeanza. Akiongea kwenye kipindi cha mchakamchaka hapa sauti ya pwani afisa msimamizi wa michezo na vijana innocent Mugabe amesema marekebisho hayo yatagarimu kaunti ya Mombasa kima cha milioni tano kabla ya awamu ya tatu kugarimu kaunti hiyo kima cha milioni kati ya kumi na ishirini.
Awamu ya pili ya uwanja huo ni kupanda nyasi na kuchimba kisima kitakachonyunyiza maji kwenye nyasi za uwanja huo na pia kusaidia timu ya michezo ya freretown fc kujikimu garama kwa uuzaji wa maji hayo kwa umma. Wakati huo huo Mgabe amesema marekebisho kama hayo yataendelea katika uwanja wa Tononoka.

 

By Japhet Makanaki