HabariMombasaSiasa

Gavana Hassan Joho ahukumiwa na mahakama ya MOMBASA…..

Mahakama ya Mombasa imemuhukumu gavana wa MOMBASA Hassan Joho kifungo cha siku 60 gerezani au alipe faini ya shilingi elfu 250 kwa kosa la kukiuka agizo la mahakama la kuzuia ubomozi wa mali ya mwanabiashara Ashock Doshi.

Akitoa agizo hilo, jaji wa mahakama hio Sila Munyao amesema kwamba Joho alikosa kuonyesha uwajibikaji na kukiuka agizo hilo licha ya cheo chake katika jamii.

Mahakama hio aidha imemtoza shilingi elfu 20 mwakilishi wadi wa wadi ya Changamwe Benard Okumu anayedaiwa kushurikiana na gavana Joho kwenye ubomozi huo huku akimuamuru kamanda wa polisi katika kaunti ya Mombasa kuwakamata mara moja wawili hao iwapo watashindwa kuthibitisha kwamba wamelipa pesa walizotozwa na kupelekwa katika gereza la Shimo la Tewa.

By Nick Waita