Habari

Familia ya mfanya Mohamed Bashir yakana madai kwamba marehemu alikuwa akijihusisha na biashara ya pesa ghushi.

Familia ya mfanya biashara raia wa Kisomali na Mmarekani Mohamed Bashir imekana madai kwamba marehemu alikuwa akijihusisha na biashara ya pesa ghushi.

Kupitia wakili wao Albaya Hassan familia hiyo imepuuza taarifa  zinazoenezwa kwamba jamaa wao alijihusisha na biashara hiyo haramu.

Hassan amesema biashara zote alizokuwa akifanya Bashir zilikuwa halali.

Hayo yanajiri huku maswali mengi yakiendelea kuzuka kuhusu kiini cha mauaji ya mfanyi biashara huyo aliyetoweka wiki mbili zilizopita na mwili wake kupatikana katika chumba cha kuhifidhi maiti katika hospitali ya Kerugoya Level 5.

Hata hivyo mwili huo utafanyiwa upasuaji hapo kesho ili kubaini jinsi alivyouliwa.

By News Desk