HabariNews

Mtoto wa Shule Afariki baada ya kuumwa na nyoka Kaunti Ya Lamu………

Huzuni imetanda kwenye familia moja eneo la Jipendeni Witu kaunti ya Lamu, baada ya mtoto wao wa darasa la pili  katika shule ya msingi ya jipendeni kufariki baada ya kuumwa na nyoka aina ya Pafada.

Pendo Katana msichana mwenye umri wa miaka 15 aliumwa na nyoka mguuni baada ya kumkanyanga alipokuwa anataka kumuua.

Mwalimu mkuu wa Jipende Peter Mwangi amesema marehemu amefariki punde tu baada ya kufikishwa katika hospitali ya Makadara mjini Mombasa ili kupokea matibabu zaidi.

Aidha familia ya mwendazake imetoa wito kwa shirika la wanyama pori KWS kuingilia kati na kuwapa fidia ya kumpoteza mwana wao.

Watu 3 wanauguza majeraha mabaya baada ya kuvamiwa na genge la waalifu katika eneo la Bomani, Likoni kaunti ya Mombasa.

Kulingana na mzee Mohamed mmoja wa waliovamiwa, alisikia kelele za nduguye na mara tu alipotoka nje kumuokoa nduguye akavamiwa na genge hilo la vijana wanaodaiwa kuwa zaidi ya kumi na waliokuwa wamejiami kwa mapanga.

Wakaazi wa eneo hilo wamelalamikia jinsi genge hilo linavyowahangaisha huku wakiitaka idara ya usalama katika eneo hilo kuingilia kati na kuhakikishia wakaazi hao usalama wa kutosha.