HabariKimataifaNews

Volkano yalipuka na kutorosha maelfu ya Familia Nchini Congo………..

Maelfu ya watu wamekimbia makazi yao katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo baada ya volkano kubwa kulipuka.

Chemchemi za lava kubwa zilitoka kwenye Mlima Nyiragongo kwa kulipuka angani usiku na kutengeneza wingu zito jekundu juu ya mji wa Goma, ambao una wakazi milioni mbili.

Mtiririko wa lava ulifika uwanja wa ndege wa jiji lakini imeripotiwa sasa umesimama.

Volkano hiyo, iliyoko 10km (maili sita) kutoka Goma, ililipuka mara ya mwisho mnamo mwaka 2002 na kuua watu 250 na kuwafanya watu wengine 120,000 kukosa makazi