HabariSiasa

Mwanamume anayedaiwa kutatiza hotuba ya rais huko Lamu kufikishwa mahakamani leo……….

Mwanamume mmoja anayedaiwa kutatiza hotuba ya rais Uhuru Kenyatta wakati wa kuzindua rasmi bandari ya Lamu katika kaunti ya Lamu siku ya alhamisi juma lililopita, bado anazuiliwa na maafisa wa usalama huku akitazamiwa kufikishwa mahakaani hii leo kujibu mashtaka dhidi yake.

James Kinywa Chomba mwenye umri wa miaka 34 anadaiwa kutatiza hotuba ya rais Kenyatta kwa sekunde kadhaa alipokuwa akihutubia umati wa wakaazi wa Lamu waliokuwa kwenye hafla ya uzinduzi wa bandari ya Lamu.

James alijitokeza kwa ghafla kumkaribia rais Kenyatta ili kuwasilisha malalamiko yake kuhusiana na ardhi kabla ya kutiwa mbararoni na maafisa wa usalama.

Mwanaume huyo ni mkaazi wa hindi eneo linalopakana na bandari hio ambapo miradi mingi ikiwemo bomba la kupitisha, barabara na reli ya kisasa zinapopitia na wakaazi wengi walipoteza ardhi zao ili kupisha miradi hio.

By Nicky Waita