HabariMazingira

Polisi Malindi walisaka kundi la vijana wahalifu…….

Maafisa wa usalama mjini malindi kaunti ya Kilifi sasa wanalisaka kundi la vijana wanaodaiwa kuhangaisha wakaazi wa mtaa wa maweni viungani mwa mji huo.

Kulingana na kamanda wa polisi eneo hilo John Kemboi  kundi hilo la kihalifu limekuwa likiwapokonya simu za mikononi wenyeji sambamba na kutekeleza vitendo vyengine vya kihalifu eneo hilo.

Kwenye taarifa yake Kemboi amesema maafisa wake watawatia mbaroni na kuwafungulia mashtaka ya uhalifu vijana hao.

Awali wenyeji eneo hilo wamekuwa wakililia usalama wao kutokana na kuchimbuka kwa kundi hilo la vijana wanaodaiwa kutumia mihadarati.

Inadaiwa uhalifu huo hutekelezwa na vijana wenye umri wa kati ya 20 na 30 na hutekeleza uhalifu huo masaa ya usiku.

 

By correspondent Joseph Yeri