HabariMombasaSiasa

Suleiman Shahbal asema hasubiri kushikwa mkono na JOHO………..

Mfanyibiashara maarufu na mwanasiasa kutoka kaunti ya Mombasa Suleiman Shahbal ameweka wazi kuwa hangojei kushikwa mkono na gavana wa kaunti ya Mombasa ili kupiga jeki uwaniaji wake wa ugavana katika kaunti hii.

Katika mahojiano ya kipekee, Shahbal ameweka wazi kuwa wanaoeneza uvumi kuwa yeye anasubiri kupokea Baraka za Joho ili apate kiti hicho wanafaa kujiandaa kisaikolojia kwani yeye anategemea mwananchi katika harakati hizo za kuwania ugavana mwaka ujao.

Lakini hata hivyo amedokeza kuwa endapo gavana Joho atakubaliana naye kimawazo na kumuunga mkono ataridhia.

Aidha ameweka wazi kuwa yeye anapania kugombania kiti cha uongozi wa Mombasa kupitia chama cha ODM huku akielezea m,atumani yake kuwa mwaka 2022 yeye ndie atakayekua kiongozi wa kaunti ya Mombasa.

 

By Warda Ahmed