HabariMombasa

Polisi Mombasa wamsaka mshukiwa wa ujambazi aliyetoroka……

Maafisa wa polisi katika kaunti hii ya Mombasa wanaendeleza msako dhido ya mshukiwa wa ujambazi ambaye aliponyoka mikononi mwa maafisa wa polisi na kisha kutoroka baada ya kukweya ukuta katika mahakama ya Mombasa.

Mshukiwa huyo   Galla Hassan anayekabiliwa na mashtaka ya mashambulizi na uwizi wa mabavu  huko Likoni alitiwa mbaroni na kufikishwa mahakamani kwa kukwepa vikao vya mahakama  baada ya kuachiliwa huru kwa dhamana.

Aidha mshukiwa huyo jana adhuhuri alidai kuenda haja na hivyo kusindikizwa na afisa wa polisi  adi chooni kisha kufunguliwa pingu,hata hivyo mshukiwa huyo alitoka chooni kwa hasira na kutumia mabavu kumusukuma hadi kumuangusha afisa huyo na kisha kutoroka juhudi za afisaa huyo kumufitulia risasi hazikufua dafu.

 

By Gladys Marura