Habari

BAADHI YA WASHUKIWA WA VISA VYA UBAKAJI UKANDA WA PWANI WANADAIWA KUPOTEA………….

Baadhi ya washukiwa wa visa vya ubakaji katika ukanda wa Pwani wanadaiwa kupotea baada ya kuachiliwa kwa dhamana na kuendeleza uovu huo.

Kwa muujibu wa kamanda mkuu wa polisi katika ukanda wa Pwani Paul Ndambuki, huenda idara ya usalama ikishirikiana na ile ya mahakama zikakosa kuwaachilia washuliwa hao na hata kuwanyima dhamana na badala yake kutumia mbinu mbadala huku akiwashauri waathiriwa wa visa hivyo kupiga ripoti kwa idara ya usalama ili wahusika wakabiliwe kwa muujibu wa sheria.

Wakati huo huo Ndambuki amewaonya baadhi ya wanainchi wanaoendeleza dhulma hizo kwamba chuma chao ki motoni huku akithibitisha kutokuwepo kwa magenge ya uhalifu yanayodaiwa kuwahangaisha wakaazi wa Pwani.

 

.BY NICK WAITA